Posts

Showing posts from February 19, 2017

TABIA YA AJABU SEHEMU-1

Image
USHINDI HATIMAYE- TABIA ZA AJABU -1 Mhubiri: Mchungaji David Mbaga Mhali: Kanisa la Waadventista Wasabato Mabatini Mwanza katika mahubiri yaliyo dhaminiwa na chama cha wanataaluma na wajasiriamali(ATAPE) Mafungu:Zaburi 14:1;Zaburi 34:21;1Samwel 25:2,3 “Mpumbavu amesema moyoni, Hakuna Mungu;Wameharibu matendo yao na kuyafanya chukizo,Hakuna atendaye mema.”(Zaburi 14:1-3) Upumbavu ni tabia ya ajabu,ambayo maandiko matakatifu Biblia yanatanabaisha kwamba Mungu anagadhabishwa nayo. Kila kunapokucha kumeendelea kuwa na watu wenye tabia za ajabu maishani.Kuona watu wa jinsi moja wakiwa katika mahusiano ya ndoa,uhalifu,utumiaji wa madawa ya kulevya,ugomvi,wizi,jamii ya watu wasio wakweli,wachoyo,mtu anachangia harusi kuliko kumchangia mtoto wa mwenzie kwenda shule, haya yote ni tabia za ajabu. Kutoisikia sauti ya Mungu ni tabia ya ajabu na Yesu alisema: “Kila mtu anayesikia maneno yangu haya na kuyatenda atafananishwa na mtu mwenye busara. kila mtu anayesikia maneno yangu h

UFAHAMU UGONJWA WA HOMA YA INI

Image
Dalili za Ugonjwa wa Homa ya INI na Jinsi Unavyoambukizwa ( Ugonjwa huu ni hatari kuliko UKIMWI) Homa  ya  Ini ni ugonjwa unaoambukizwa kwa njia ya virusi ambavyo vikishaingia mwilini hushambulia ini kabla ya kugeuka maradhi sugu.Virusi hivyo vinaitwa HBV (Hepatitis B Virus). Virusi hivyo husambazwa kwa njia ya damu au majimaji mengine ya mwilini, mfano mate au jasho. Watu takriban 1,000,000 wanapoteza maisha duniani kote kutokana na ugonjwa wa Homa ya Ini (Hepatitis B). Ugonjwa huu kama haujatibiwa hutengeneza uvimbe katika ini na kusababisha kansa ya ini na baadaye Kifo. JINSI  UNAVYOAMBUKIZWA: Katika maeneo hatari zaidi duniani, Virusi vya Hepatitis B (HBV) kwa kawaida husambazwa kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto wakati wa kuzaliwa au kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine hususan nyakati za utotoni. Kama ilivyo kwa Ukimwi, Virusi vya Homa ya Ini pia huambukizwa kwa njia ya kujamiiana, mate, jasho na mwingiliano wowote ule wa damu. Njia  kuu  za  maambuk

MTAALAMU WA MAABARA PITA HAPA

Image