TABIA YA AJABU SEHEMU-1


USHINDI HATIMAYE- TABIA ZA AJABU -1
Mhubiri: Mchungaji David Mbaga
Mhali: Kanisa la Waadventista Wasabato Mabatini Mwanza katika mahubiri yaliyo dhaminiwa na chama cha wanataaluma na wajasiriamali(ATAPE)
Mafungu:Zaburi 14:1;Zaburi 34:21;1Samwel 25:2,3
“Mpumbavu amesema moyoni, Hakuna Mungu;Wameharibu matendo yao na kuyafanya chukizo,Hakuna atendaye mema.”(Zaburi 14:1-3)
Upumbavu ni tabia ya ajabu,ambayo maandiko matakatifu Biblia yanatanabaisha kwamba Mungu anagadhabishwa nayo. Kila kunapokucha kumeendelea kuwa na watu wenye tabia za ajabu maishani.Kuona watu wa jinsi moja wakiwa katika mahusiano ya ndoa,uhalifu,utumiaji wa madawa ya kulevya,ugomvi,wizi,jamii ya watu wasio wakweli,wachoyo,mtu anachangia harusi kuliko kumchangia mtoto wa mwenzie kwenda shule, haya yote ni tabia za ajabu.
Kutoisikia sauti ya Mungu ni tabia ya ajabu na Yesu alisema: “Kila mtu anayesikia maneno yangu haya na kuyatenda atafananishwa na mtu mwenye busara. kila mtu anayesikia maneno yangu haya na hayatendi atafananishwa na mtu mpumbavu.(Mathayo 7:24-27)
Mwenyezi Mungu alisema “Usiwe na miungu mingine ila MIMI’’ (Kutoka 20:1-2). Chochote kisichokuwa cha Roho Mtakatifu ni miungu mbele za Mungu. Chochote kinachochukua nafasi ya Mungu katika maisha yako ni miungu mbele za Mungu.Yaweza kuwa ni tumbo lako ambalo unalitumikia hata kumsahau Mungu wako.Tumeshindwa kumwabudu Mungu wetu na kufuata mambo yetu wenye,hii ni tabia ya ajabu na kwa Mungu ni upumbavu.
Kwa maana MUNGU pekee ndiye astahili kuabudiwa,tunamwabudu Mungu si kwasababu tunataka kwenda Mbinguni bali tunamwabudu Mungu muumbaji wetu kwakuwa Yeye pekee anastahili kuabudiwa na kila kiumbe.Mungu aliposema siku ya saba ni kupumzika(Mwanzo 2:1-2)lakini mpumbavu yeye husema,ibada ni ibada tuu;Mgogoro si siku ya sabato,mgogoro ni ibada.Mungu anapotoa maelekezo isikilize sauti yake nawe ukaishi.
Yupo Roho Mtakatifu katika kutusaidia kuisikia sauti ya Mungu. Hivyo jenga na kudumisha uhusiano wako na Yeye, itakusaidia sana katika kiujua na kuisikia sauti ya Mungu

Comments

Popular posts from this blog

UFAHAMU UGONJWA WA HOMA YA INI

FUNGULIA MORNING STAR MNAMO SAA 12:00 JIONI