UFAHAMU UGONJWA WA HOMA YA INI
Dalili za Ugonjwa wa Homa ya INI na Jinsi Unavyoambukizwa ( Ugonjwa huu ni hatari kuliko UKIMWI) Homa ya Ini ni ugonjwa unaoambukizwa kwa njia ya virusi ambavyo vikishaingia mwilini hushambulia ini kabla ya kugeuka maradhi sugu.Virusi hivyo vinaitwa HBV (Hepatitis B Virus). Virusi hivyo husambazwa kwa njia ya damu au majimaji mengine ya mwilini, mfano mate au jasho. Watu takriban 1,000,000 wanapoteza maisha duniani kote kutokana na ugonjwa wa Homa ya Ini (Hepatitis B). Ugonjwa huu kama haujatibiwa hutengeneza uvimbe katika ini na kusababisha kansa ya ini na baadaye Kifo. JINSI UNAVYOAMBUKIZWA: Katika maeneo hatari zaidi duniani, Virusi vya Hepatitis B (HBV) kwa kawaida husambazwa kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto wakati wa kuzaliwa au kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine hususan nyakati za utotoni. Kama ilivyo kwa Ukimwi, Virusi vya Homa ya Ini pia huambukizwa kwa njia ya kujamiiana, mate, jasho na mwingiliano wowote ule wa damu. Njia kuu za maambuk
Comments
Post a Comment